Wednesday, July 2, 2014

MESS JACOB CHENGULA NA EMMANUEL MABISA WAKITANGAZA INJILI VIJINI

Baada ya kufanya kazi ya Mungu mikoa mbalimbali na hasa mijini, sasa watumishi wa Mungu wameamua kuwafata kondoo waliopotea huko vijijini na kuwarudisha kundini. Hii inatia moyo sana kuona watumishi wa Mungu wanaachia jiji na kukimbilia vijijini wakiwa na nguvu kwa lengo la kumtumikia Mungu.

Mess Jacob Chengula na Emmanuel Mabisa waliingia katika kijiji kimoja mkoa wa Dodoma kwa kazi moja tu ya kumuimbia Bwana Yesu Kristo na kuhakikisha ujumbe waliobeba kwa njia ya uimbaji unawafikiwa wanakijiji.

Mess Jacob Chengula (kulia)

Waimbaji tunatakiwa kutambua kuwa tumepewa kazi ya kumtumikia Mungu kwa mali zetu, akili zetu na karama zetu bila ya malipo. Tuache kile kiroho kinachotusukuma kutamani pesa na kuacha ule wito wetu. Imefika kipindi mwimbaji anakataa kwenda kuimba eti pesa aliyoambiwa na mtumishi ni ndogo kwa hiyo hawezi kwenda kuimba. Jamani tuache kuweka Injili kama biashara, ipo siku tutatoa hesabu.

Emmanuel Mabisa

Waimbaji wamekuwa ni watu wa kutaka pesa nyingi sana kutoka kwa watumishi wa Mungu. Utakuta mwimbaji anasema mimi siwezi kwenda kuimba kama huna milioni moja au milioni mbili. Hii haipendeza kabisa watu wa Mungu, tunatakiwa kujirekebisha. Tunatambua ya kwamba tunahitaji pesa lakini isiwe kwa kupitia Injili.

Ushauri wangu kwa waimbaji ni kwamba. Muombe Mungu akupe biashara au kazi yoyote nje ya uimbaji ili Mungu aweze kufungua milango ya mafanikio katika hiyo kazi ya mikono yako. Mungu atakubariki kwasababu wewe umeamua kumuimbia Mungu wako bila ya kuangalia maslahi. Mungu atakupa wateja wengi sana katika biashara yako kwasababu unafanya kazi ya YAKE kwa uaminifu na kwa moyo wote.

Wako Katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAAFRICA. FOR ALL NATIONS
www.rumaafrica.blogspot.com





KAMA ANN ANNIE NASEMA MBEYA GOSPEL FESTIVAL 2014 HAISIMULIKI...

Mimi kama Ann Annie ninamshukuru Mungu kwanza kwa kuniwezesha kushiriki katika Tamasha kubwa sana jijini Mbeya linaloenda kwa jina la Mbeya Gospel Festival. Niliweza kuuona utukufu wa Mungu kwa kupitia uimbaji wa wenzangu niliokuwa nao katika tamasha hili la kipekee.

Tamasha hili lilihudhuria na watu wengi sana ambapo nilishindwa kushangaa na nikabaki mdomo wazi. Nilichojifunza ni kwamba kumbe watu wanaohitaji Injili ni wengi lakini watenda kazi ni wachache.

Tamasha hili liliandaliwa na Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania kwa lengo la kuwahimiza wakazi wa mkoa wa Mbeya kujiunga na chama hicho ili waweza kujua haki zao za Muzikia na pia kuleta mshikamano na ushirikiano kati ya waimbaji.

 kushoto ni Ann Annie

Ann Annie akifanya mambo kwa utukufu wa Mungu

 Ann Annie katikati na waimbaji wenzake (kulia ni Rachel Sharp)
 Rachel Sharp
 Emmanuel Mabisa
 Mwasomola
 Mess Jacob Chengula aliyevalia koti jeupe


Saturday, June 28, 2014

VUNJIKA MBAVU NA KING MAJUTO NDANI YA FILAMU YA INSIDE

Filamu hii Jennifer Kyaka (Odama) ambayo inayonyesha maisha ya wafanyakazi maofisi wanaovyofanya vituko na mabosi wao na wengine hata kumkufuru na kumuudhi Mungu kwa vitendo vya rushwa na uvivu kazini, kwa mana Mungu amesema asiyefanya kazi na asile. Watu badala ya kufanya kazi wanabaki kupiga stori na majungu maofisi. Wadada wanavyotumia uzuri wao kuwalaghai waume za watu kwa kutoa rushwa ya ngono. Hakika kama mcha Mungu ndani ya hii filamu utajifunza mengi na utaburudika na vituko vya wasanii maarufu wa kuchekesha kama KING MAJUTO na  BENY, pia utamuona marehemu RACHEL HAULE, DAVINA, ODAMA, DULLAH WA PLANET BONGO, na wengine wemgi sana. Filamu hii ambayo imetengezwa na kampuni bora Tanzania ya J-FILM 4 LIFE itakuweka mahali fulani KIMAWAZO.

Tuesday, April 15, 2014

MTU NA KAKA YAKE, GRACE NA JOSHU KUACHIA ALBAMU YAO YA KWANZA YA MY SAVIOUR GOD

Baada ya kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali, Grace na Joshu wameamua sasa kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu. Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya albamu yao hii ya kwanza.

Grace Christian Rwegasha

Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili  ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.

Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao  ya uimbaji.

Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.

Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha

Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.

Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi  ya Bwana.

Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.

Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080

MUNGU AKUBARIKI

Monday, April 14, 2014

MKE WA MWIMBAJI ALIYEFARIKI NCHINI KENYA AJIFUNGUA MDA MCHACHE BAADA YA MAZISHI YA MUMEWE



Marehemu Peter Kaberere na mkewe enzi za uhai wake.© Kaberere Facebook

Mke wa mwimbaji wa muziki wa injili nchini Kenya marehemu Peter Kaberere ambaye amefariki wiki iliyopita wakati akiosha gari yake, mkewe amejifungua mtoto wa kike masaa machache baada ya mazishi ya mwimbaji huyo siku ya ijumaa iliyopita.

Mke wa marehemu aitwaye Mary Njeri au wengi hupenda kumwita Njesh alikuwa mjamzito wa kukaribia kujifungua wakati mmewe alipofariki wiki iliyopita. Tayari wanandoa hao walikuwa na mtoto wa kiume kabla ya baraka nyingine ya mtoto wa kike ambaye amezaliwa wakati ambao mwimbaji huyo ameshaaga dunia.

Kusoma chanzo cha kifo cha mwimbaji huyo BONYEZA HAPA.

Tuesday, April 8, 2014

ANNIE ANNA AFUNGU BLOGU YAKE SIKU YA LEO JUMANNE 8/4/2014

Bwana Yesu asiwe, nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali siku ya leo. Nimemuona Mungu akinitete tangi siku nimeliona jua hapa dunia mpaka sasa. Mungu amezidi kuwa mwaminifu kwangu na amekuwa akitimizia haja ya moyo wangu. Nimemuona Mungu akipandisha kila kuitwapo leo, ameibariki huduma yangu ya uimbaji. Na siku ya leo amenipa kibali cha kuweza kumiliki blogu yangu hii ambayo itafanyika madhabahu ya Mungu.

Mwimbaji Annie Anna
Kwa kupitia blogu hii watu wataokoka na watamrudia Mungu hasa pale watakaposoma yale ambayo Mungu ameniambia niyaandike kwaajili yako na wao.

Hello Mpendwa ningependa kukukaribisha katika blogu yangu mpya mabyo siku ya leo Jumanne 8/4/2014 nimeiachia hewani. Blogu yangu itajikita zaidi kuelezea maendeleo ya huduma yangu ya uimbaji na huduma zingine nazitoa, pia habari mbalimbali za kumuinua Kristo. Tutakuwa na maanda mbalimbali kutoka kwa waimbaji wenzangu, wachungaji, Manabii, Mitume, waalimu na Wainjilisti.
Mwimbaji Annie Anna

Ninaamini utafurahia sana kile nitakachokuwa nakumegea kwa ufalme wa Mungu. Pia ninategemea kujifunza mengi sana kutoka kwako, kwani katika blogu hii utakuwa na uwezao wa kututumian kile ambacho ungependa tushirikiane kumtukuza Mungu.
 Mwimbaji Annie Anna
Wachungaji na watumishi mbalimbali watatpata muda wa kuweza kuweka mahubiri yao kutoka katika makanisa yao au mikutano yao. Tunatambua ya kwamba kuna watu wanaoishi mbali na huduma yako na hawajabahatika kupata huduma yako, lakini kwa kupitia blogu hii wataweza kupata kile ambacho umekihubiri kanisani kwako au katika mkutano uliohudhuria.

Mwimbaji Annie Anna
 Tutakuwa na maada za kijamii zenye kumtukuza Mungu. Watu mbalimbali bila ya kuchagua dini wala kabiala wataweza kuchangia kile ambacho wanaona kitamfaa Mtanzania na mtu yeyote yule atakapokisoma. Tunatambua ya kwamba Mungu amempa kila mtu karama yake kwa kazi yake kwahiyo blogu hii itajitahidi kutafuta watu wa namna hii ili kuweza kupata mchango wao

Mwimbaji Annie Anna
 Pia tutaweza kuwashirikisha waalimu wanaofundisha Neno la Mungu kutoka kila kona ya makanisa ili waweze kutoa mafundisho yao kwa kupitia blogu yetu hii. Hakika ninaamini kwa kupitia blogu hii, Mungu atafanya jambo katika maisha yako.

Mwimbaji Annie Anna
 
Mwimbaji Annie Anna

Annie Anna

















 

MWIMBAJI W NYIMBO ZA INJILI TANZANIA ANNIE ANNA ALIVYOSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA SHUKRANI LA MESS JACOB CHENGULA SIKU YA JUMAPILI 30.03.2014


 Annie Anna Isaac

 Annie Anna Isaac

Baada ya kufanta uzinduzi wake wa albamu ya MUNGU HABADILIKI Mess Jacob Chengula aliweza kuweka tamasha la kumshukuru Mungu katika kanisa la KKKT Mbezi Kimara. Watu walikuwa ni wengi sana waliofika mahali pale kwa lengo la kuungana na mwimbaji huyu katika kazi ya Bwana. Mess Jacob Chengula aliongozana na waimbaji wengi na moja wapo ni Bony Mwaitege, Manesa Sanga, Elizabeth Ngaiza, Stella Joel, Annie Anna Isaac kutoka Moshi, Joshua Makondeko na wengine wengi. Tamasha lilikuwa zuri sana na watu walibaroikiwa na uimbaji wa watumishi hawa wa Mungu.
Mess Jacob Chengiula alimshukuru sana Mungu kwa kupata kibali cha kuweza kufanikisha tamasha hili la shukrani pamoja na kuwapongeza wachungaji, wazee wa kanisa na waumini wa kanisa hilo kwa kumruhusu kufanya kazi ya Bwana kanisani hapo.
TUONE MATUKIO KATIKA PICHA
 Kulia ni Joshua Makondeko akiwa na Bony Mwaitege
 Joshua Makondekoakimtukuza Mungu
 Stella Joel
 Stella Joel

 Bony Mwaitege
 Bony Mwaitege
 Elizabeth Ngaiza
 Manesa Sanga
 Mess Jacob Chengula akiingia kanisani kwa kazi ya Bwana

 Mess Jacob Chengula, Manesa Sanga na dancers wake wakimtukuza Mungu siku hii
 Mess Jacob Chengula na dancers wake wakimtukuza Mungu siku hii
You might also like: