Tuesday, April 8, 2014

ANNIE ANNA AFUNGU BLOGU YAKE SIKU YA LEO JUMANNE 8/4/2014

Bwana Yesu asiwe, nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kunipa kibali siku ya leo. Nimemuona Mungu akinitete tangi siku nimeliona jua hapa dunia mpaka sasa. Mungu amezidi kuwa mwaminifu kwangu na amekuwa akitimizia haja ya moyo wangu. Nimemuona Mungu akipandisha kila kuitwapo leo, ameibariki huduma yangu ya uimbaji. Na siku ya leo amenipa kibali cha kuweza kumiliki blogu yangu hii ambayo itafanyika madhabahu ya Mungu.

Mwimbaji Annie Anna
Kwa kupitia blogu hii watu wataokoka na watamrudia Mungu hasa pale watakaposoma yale ambayo Mungu ameniambia niyaandike kwaajili yako na wao.

Hello Mpendwa ningependa kukukaribisha katika blogu yangu mpya mabyo siku ya leo Jumanne 8/4/2014 nimeiachia hewani. Blogu yangu itajikita zaidi kuelezea maendeleo ya huduma yangu ya uimbaji na huduma zingine nazitoa, pia habari mbalimbali za kumuinua Kristo. Tutakuwa na maanda mbalimbali kutoka kwa waimbaji wenzangu, wachungaji, Manabii, Mitume, waalimu na Wainjilisti.
Mwimbaji Annie Anna

Ninaamini utafurahia sana kile nitakachokuwa nakumegea kwa ufalme wa Mungu. Pia ninategemea kujifunza mengi sana kutoka kwako, kwani katika blogu hii utakuwa na uwezao wa kututumian kile ambacho ungependa tushirikiane kumtukuza Mungu.
 Mwimbaji Annie Anna
Wachungaji na watumishi mbalimbali watatpata muda wa kuweza kuweka mahubiri yao kutoka katika makanisa yao au mikutano yao. Tunatambua ya kwamba kuna watu wanaoishi mbali na huduma yako na hawajabahatika kupata huduma yako, lakini kwa kupitia blogu hii wataweza kupata kile ambacho umekihubiri kanisani kwako au katika mkutano uliohudhuria.

Mwimbaji Annie Anna
 Tutakuwa na maada za kijamii zenye kumtukuza Mungu. Watu mbalimbali bila ya kuchagua dini wala kabiala wataweza kuchangia kile ambacho wanaona kitamfaa Mtanzania na mtu yeyote yule atakapokisoma. Tunatambua ya kwamba Mungu amempa kila mtu karama yake kwa kazi yake kwahiyo blogu hii itajitahidi kutafuta watu wa namna hii ili kuweza kupata mchango wao

Mwimbaji Annie Anna
 Pia tutaweza kuwashirikisha waalimu wanaofundisha Neno la Mungu kutoka kila kona ya makanisa ili waweze kutoa mafundisho yao kwa kupitia blogu yetu hii. Hakika ninaamini kwa kupitia blogu hii, Mungu atafanya jambo katika maisha yako.

Mwimbaji Annie Anna
 
Mwimbaji Annie Anna

Annie Anna

















 

No comments:

Post a Comment