Wednesday, July 2, 2014

MESS JACOB CHENGULA NA EMMANUEL MABISA WAKITANGAZA INJILI VIJINI

Baada ya kufanya kazi ya Mungu mikoa mbalimbali na hasa mijini, sasa watumishi wa Mungu wameamua kuwafata kondoo waliopotea huko vijijini na kuwarudisha kundini. Hii inatia moyo sana kuona watumishi wa Mungu wanaachia jiji na kukimbilia vijijini wakiwa na nguvu kwa lengo la kumtumikia Mungu.

Mess Jacob Chengula na Emmanuel Mabisa waliingia katika kijiji kimoja mkoa wa Dodoma kwa kazi moja tu ya kumuimbia Bwana Yesu Kristo na kuhakikisha ujumbe waliobeba kwa njia ya uimbaji unawafikiwa wanakijiji.

Mess Jacob Chengula (kulia)

Waimbaji tunatakiwa kutambua kuwa tumepewa kazi ya kumtumikia Mungu kwa mali zetu, akili zetu na karama zetu bila ya malipo. Tuache kile kiroho kinachotusukuma kutamani pesa na kuacha ule wito wetu. Imefika kipindi mwimbaji anakataa kwenda kuimba eti pesa aliyoambiwa na mtumishi ni ndogo kwa hiyo hawezi kwenda kuimba. Jamani tuache kuweka Injili kama biashara, ipo siku tutatoa hesabu.

Emmanuel Mabisa

Waimbaji wamekuwa ni watu wa kutaka pesa nyingi sana kutoka kwa watumishi wa Mungu. Utakuta mwimbaji anasema mimi siwezi kwenda kuimba kama huna milioni moja au milioni mbili. Hii haipendeza kabisa watu wa Mungu, tunatakiwa kujirekebisha. Tunatambua ya kwamba tunahitaji pesa lakini isiwe kwa kupitia Injili.

Ushauri wangu kwa waimbaji ni kwamba. Muombe Mungu akupe biashara au kazi yoyote nje ya uimbaji ili Mungu aweze kufungua milango ya mafanikio katika hiyo kazi ya mikono yako. Mungu atakubariki kwasababu wewe umeamua kumuimbia Mungu wako bila ya kuangalia maslahi. Mungu atakupa wateja wengi sana katika biashara yako kwasababu unafanya kazi ya YAKE kwa uaminifu na kwa moyo wote.

Wako Katika Bwana
Rulea Sanga
RUMAAFRICA. FOR ALL NATIONS
www.rumaafrica.blogspot.com





KAMA ANN ANNIE NASEMA MBEYA GOSPEL FESTIVAL 2014 HAISIMULIKI...

Mimi kama Ann Annie ninamshukuru Mungu kwanza kwa kuniwezesha kushiriki katika Tamasha kubwa sana jijini Mbeya linaloenda kwa jina la Mbeya Gospel Festival. Niliweza kuuona utukufu wa Mungu kwa kupitia uimbaji wa wenzangu niliokuwa nao katika tamasha hili la kipekee.

Tamasha hili lilihudhuria na watu wengi sana ambapo nilishindwa kushangaa na nikabaki mdomo wazi. Nilichojifunza ni kwamba kumbe watu wanaohitaji Injili ni wengi lakini watenda kazi ni wachache.

Tamasha hili liliandaliwa na Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania kwa lengo la kuwahimiza wakazi wa mkoa wa Mbeya kujiunga na chama hicho ili waweza kujua haki zao za Muzikia na pia kuleta mshikamano na ushirikiano kati ya waimbaji.

 kushoto ni Ann Annie

Ann Annie akifanya mambo kwa utukufu wa Mungu

 Ann Annie katikati na waimbaji wenzake (kulia ni Rachel Sharp)
 Rachel Sharp
 Emmanuel Mabisa
 Mwasomola
 Mess Jacob Chengula aliyevalia koti jeupe